Rais Jakaya Mrisho Kikwete
amewasili Brussels, Ubelgiji jana asubuhi 2 Aprili,2014 kuhudhuria kikao
cha siku mbili cha Wakuu wa Nchi wa nchi za Afrika na za Umoja wa Ulaya (EU-Africa Summit)
Kikao hiki cha siku 2
kitatoa nafasi kwa viongozi hawa kutathmini mafanikio ya uhusiano wao
na kutafuta njia zingine mpya za kuboresha mahusiano hayo .
Kauli mbiu ya mkutano wa Mwaka
huu inasisitiza katika kuwekeza kwa watu,Mafanikio na Amani (Investing in
people, prosperity and peace) na baadaye kufanya mazungumzo na Rais wa
Kamisheni wa Nchi za Ulaya (EU) Bw. Jose Manuel Barosso.
Akiwa Brussels Rais Kikwete
anatarajia kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban
Ki Moon na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mheshimiwa Mark Rutte.
Rais Kikwete anatarajia kuondoka
Brussels mara baada ya Mkutano kumalizika na kurejea Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment