Home » » KINANA ASUGUA KICHWA ALIPOTEMBELEA MPAKA WA TANZANIA NA BURUNDI

KINANA ASUGUA KICHWA ALIPOTEMBELEA MPAKA WA TANZANIA NA BURUNDI

Written By kitulofm on Friday, 11 April 2014 | Friday, April 11, 2014


Watu wakivuka Mto Malagarasi wakitokea Burundi ambako huuza na kununua bidhaa zao kwenye soko la mchana maarufu kama soko la Buhija.

.Asimama kwa dakika 20 kuangalia shughuli za kila siku mpakani mwa Tanzania na Burundi, ajiuliza maswali mengi na kupata majibu, atoa ushauri kwa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.
.Ajionea maisha halisi ya watu wa mpakani mwa Tanzania na Burundi
.Ashindwa kuelewa kwa nini soko la mifugo lilikufa
.Ashangaa viongozi kutokuwa wabunifu hasa katika fursa zinazoweza kuwasaidia wananchi
Untitled
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amesimama mpakani mwa Tanzania na Burundi katika kijiji cha Kibande wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma akiangalia upande wa Burundi kwenye kijiji cha Murambi.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na viongozi wa CCM mkoa wa Kigoma kuelekea kwenye mkutano wa hadhara baada ya kushuhudia mfumo mzima wa maisha ya mpakani mwa Tanzania na Burundi.
 Hili ndio soko la mchana la Buhija ambapo Watanzania wengi wanaoishi wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma hufanya shughuli zao za biashara, soko hili lipo nchini Burundi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikata muwa ambao aliununua kutoka kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa mpakani mwa Tanzania na Burundi
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm