Watu sita wameuawa na wengine 25 kujeruhiwa vibaya
katika shambulizi la kigaidi katika eneo la California mtaa wa
Eastleigh, viungani mwa mji wa Nairobi.
Kamanda wa Polisi mjini Nairobi Benson Kibue
amesema kuwa milipuko miwili ilitokea wakati magaidi waliporusha
vilipuzi katika mikahawa miwili midogo.
Mlipuko wa tatu ulitokea katika kituo cha mabasi ya uchukuzi kilichoko karibu na zahanati za afya ya mama na mtoto.
0 comments:
Post a Comment