Home » » MAJONZI:ABIRIA WALIONUSURIKA KIFO KWENYE AJALI YA MELI KOREA KUSINI WASIMULIA JINSI ILIVYOTOKEA

MAJONZI:ABIRIA WALIONUSURIKA KIFO KWENYE AJALI YA MELI KOREA KUSINI WASIMULIA JINSI ILIVYOTOKEA

Written By kitulofm on Wednesday, 16 April 2014 | Wednesday, April 16, 2014

Watu walionusurika kifo katika ajali ya meli nchini Korea Kusini wamekuwa wakielezea hali ilivyokuwa ya kutisha ndani ya meli ya Korea Kusini ilipoanza kusimama kwa kuyumba, ikiegemea upande mmoja na haraka kuanza kuzama.

"Kwa kweli kulikuwa na sauti kubwa na meli ghafla ikanza kuegemea upande mmoja," amesema abiria aliyeokolewa, Kim Song-Muk.
"watu walikuwa wakihangaika kukimbilia maeneo ya juu ya meli, lakini ilikuwa vigumu kufanya hivyo kutokana na meli kupinduka."

Bado haijafahamika kilichosababisha kuzama kwa meli hiyo, ambayo kwa kiasi kikubwa iliwabeba wanafunzi wa shule, lakini watu walionusurika katika ajali hiyo wanatoa maelezo sawa kuhusu tukio hilo la kutisha.

Kikosi cha Walinzi wa Pwani ya Korea Kusini kimesema abiria wapatao mia tatu hawajulikani walipo baada ya meli kupinduka na kuzama.

Watu wawili wamefahamika kupoteza maisha na watu mia moja na sitini na wanne wameokolewa. Kikosi cha wapiga mbizi kwa sasa wanatafuta meli iliyozama.

Wengi wa abiria wa meli hiyo ni wanafunzi wa sekondari wakiwa katika safari ya masomo kuelekea kisiwa cha Jeju, nchini Korea Kusini.

Meli hiyo ilikuwa na watu 460. Zaidi ya miatatu hawajapatikana, wengine 164 wameokolewa na wengine wawili wamethibitishwa kufariki.

CHANZO:BBC
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm