Home » » MATUKIO YA MAUAJI MBEYA YARINDIMA MLINZI AUAWA AKIWA KAZINI

MATUKIO YA MAUAJI MBEYA YARINDIMA MLINZI AUAWA AKIWA KAZINI

Written By kitulofm on Wednesday, 9 April 2014 | Wednesday, April 09, 2014

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya Limethibitisha  Kutokea  Kwa tukio  la Kifo cha Mlinzi Mmoja wa Kampuni Binafsi  Aliyefahamika Kwa Jina La Hamisi Ramadhan Mwenye Umri wa Miaka 50  Mkazi Wa Sogea.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya Imeeleza Kua Mlinzi Huyo  Aliuawa Kwa Kupigwa Na Kitu Kizito Kichwani Na Watu Wanaosadikiwa Kuwa Ni Wezi Akiwa Kazini na Kwamba Tukio Hilo Limetokea Usiku Wa Kuamkia Aprili Nane Mwaka huu Majira Ya Saa Nane na Robo .

Aidha Taarifa Hiyo Imefafanua Kuwa Mauaji Hayo Yametokea Huko Katika Eneo La Msikitini Tunduma, Kata Na Tarafa Ya Tunduma, Wilaya Ya Momba, Mkoa Wa Mbeya.

Inadaiwa Kuwa, Watu Hao Kabla Ya Kutekeleza Mauaji Hayo, Walimvizia Mhanga Wakati Amekaa Kwenye Veranda Moja Wapo Kati Ya Maduka Mawili Anayolinda Akiota Moto Na Kisha Kumpiga.

Watu Hao Wanadaiwa Kuvunja  Maduka Mawili [Duka La Dawa Na Duka La Furniture] Kwa Lengo La Kuiba Lakini Hawakufanikiwa Kuchukua Kitu Chochote Kwani Walinzi Wa Maduka Jirani Walitoa Taarifa Kwa Askari Wa
Doria Ambao Walianza Kuwakimbiza Wezi Hao Na Kuelekea Chianga – Nakonde Zambia.

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi  Ahmed   Msangi Amesema Msako Mkali Unaendelea Kwa Ushirikiano Kati Ya Polisi Wa Tunduma Na Nakonde Ili Kuwakamata Watuhumiwa Hao Ambao Wametokea Eneo Hilo.

Hadi Sasa Mwili Wa Marehemu Umehifadhiwa Kituo Cha Afya Tunduma huku Jeshi la Polisi Likitoa Wito Kwa  Yeyote Mwenye Taarifa Za Mahali Walipo Watuhumiwa Wa Tukio Hilo Wazitoe  Katika Mamlaka Husika Ili Wakamatwe Na Hatua Za Kisheria Zichukuliwe Dhidi Yao
CHANZO:EDDY BLOG
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm