Mtu
mmoja mkazi wa kijiji cha Masisiwe kata ya Ukwama Wilayani Makete Mkoani Njombe
amefariki baada ya kupingwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mguuni na Mtu/watu
wasiojulikana mwishoni mwa wiki iliyopita
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Mrakibu mwandamizi wa Polisi Wilaya ya Makete kwa niaba
ya Kamanda wa Polisi Wilaya Bw.Gozbert Komba
amesema walipokea taarifa kutoka katika uongozi wa kijiji hicho na
kumtaja marehemu kuwa ni Masori Sanga(60) mkazi wa kijiji cha Masisiwe Kata ya
Ukwama Wilayani Makete
Komba
amesema kuwa marehemu huyo aliuawa usiku wa kuamikia ijumaa wiki iliyopita na
watu wasiojulikana kwa imani za kishirikina
Pia
amesema mpaka sasa Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi kwa ajili ya kuhakikisha
wahusika wote watukio hilo wanakamatwa kwani kitendo walichokifanya ni cha
kinyama na baada ya tukio hilo muuaji/wauaji
hao walitokomea kusiko julikana
Bw.Komba
amekemea vikari suara la wananchi wengi
kujichukulia sheria mkononi wilayani Makete na kuwaomba wananchi wasiwe na
tabia hizo za kuwaua wazee kwa imani za kishirikina na kuwataka watiii sheria bila
shuruti ili kuishi kwa Amani katika wilaya yao na nchini kwa ujumla
0 comments:
Post a Comment