Picha kwa Idhaa ya Eddy Blog
Moto umeteketeza vibanda vya biashara viwili mali ya Bw.Edson Tweve na Denyelela Mahenge katika kijiji cha Isapulano Kata ya Isapulano wilayani Makete Mkoani Njombe usiku wa kuamkia leo mnamo saa 6 usiku hadi saa 9 Usiku
Moto umeteketeza vibanda vya biashara viwili mali ya Bw.Edson Tweve na Denyelela Mahenge katika kijiji cha Isapulano Kata ya Isapulano wilayani Makete Mkoani Njombe usiku wa kuamkia leo mnamo saa 6 usiku hadi saa 9 Usiku
Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu Bw. Kumbusho Mhenge kutoka katika kijiji hicho amesema "Tukio hilo linasemekana kuhusika na Mtu/watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo katika kijiji hicho ambapo mashuhuda wa tukio wameelezea jinsi walivyoshuhudia kuwa Kibanda kimoja cha Bw.Edson Tweve kilibomolewa na kumwagiwa Mafuta aina ya Petrol na kuwashwa moto ambapo ulipamba katika chumba cha jirani na moto kuendelea kurindima"
"Niligundua kuwaka kwa moto huo mnamo saa 6 hivi usiku katika kibanda changu lakini sikuwa na hofu zaidi kwani nilijua huenda ni moshi wa kawaida, lakini ilipofika saa 9 usiku nikamwamsha mume wangu ndipo tulianza safari za kuelekea hapo tukakuta kibanda kimeteketea chote kwa moto na kuanza kupiga mayowe kwa majirani"Alisema Mke wa Bw.Edson
Hata hivyo taarifa ilitolewa katika kituo cha Polisi ambapo walifika katika eneo la tukio lakini hakuna mtu yeyote aliyekamatwa wala kuhisiwa na tukio hilo hadi sasa
"Uongozi wa kijiji nao umesema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha na kutishia amani iliyopo kijijini hapa na kila mmoja wetu ni vema akawa Mpelelezi ili kufanikisha kuwakamata wahalifu hao"Alisema Bw.Kumbusho Mhenge
Msomaji wa Mtandao huu tutaendelea kukujulisha kwa kadri tutakavyokuwa tunazipata habari hizi kwa Undani zaidi
Na Furahisha Nundu
0 comments:
Post a Comment