Kumeibuka ongezeko la
waganga wa jadi wilayani Makete mkoani Njombe ambao wamekuwa wakijitangaza kwa
kuweka mabango yao ya kujinadi katika nguzo za umeme licha ya sheria na kanuni
kukataza wao kujitangaza kwa njia hiyo
Akizungumza na kitulo
fm mapema hii leo afisa afya wilayani makete bwana bonifas sanga amesema
kisheria na kanuni inakataza kutangaza kujitangaza kwa kuweka
mabango.
Amesema mganga yoyote
anaefika makete anatakiwa kuonana na mganga mkuu wa wilaya ili haweze
kukaguliwa vibali vyake kabla ya kuanza kufanya kazi au kutoa tiba na yeye
bwana afya anatakiwa kwenda kukagua sehemu ambazo wanafanyia kazi.
Aidha Bwana sanga
amesema wataendelea kuwafatilia waganga wa hao wa tiba asili kwa ukaribu na
watatoa taarifa kwa wananchi na kuomba wakazi wa makete kuacha tabia ya
kukurupukia waganga hao wasio wafahamu wanakotoka.
0 comments:
Post a Comment