Home » » MTOTO WA MIAKA MINNE ABAKWA, AUMIZWA VIBAYA

MTOTO WA MIAKA MINNE ABAKWA, AUMIZWA VIBAYA

Written By kitulofm on Wednesday, 9 April 2014 | Wednesday, April 09, 2014

Iddi Mgosi anashikiliwa na Polisi wa Kituo cha Wazo jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka minne (jina linahifadhiwa) huko Mivumoni, Madale Machi 18, mwaka huu.

Mgosi, ambaye umri wake haukuweza kupatikana mara moja, anadaiwa kumrubuni mtoto huyo kutoka nyumbani kwao na kumpeleka kwake, ambako alimuingilia kwa nguvu na baadaye kumtisha kutosema lolote kwa wazazi wake.

Mama mzazi wa mtoto huyo, aligundua mwanaye kuwa na maumivu makali wakati akimuogesha, kwani alipomshika sehemu zake za siri, binti huyo alipiga kelele za maumivu na alipoulizwa kilichomsibu ndipo alipoelezea alichofanyiwa.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa, mama huyo aitwaye Hadija, alisema alikuwa akimuogesha mtoto wake huyo bila kugundua kwamba alikuwa amebakwa na kuharibiwa vibaya sehemu zake za siri. Alipomshika kwa ajili ya kumsafisha, mtoto huyo akaanza kulia na kulalamika kwamba alikuwa akimuumiza.

Bi Hadija alisema mara baada ya kuambiwa hivyo, akawaita ndugu zake na kuwasimulia alichoambiwa hivyo wote kwa pamoja wakachukua jukumu la kumfuata Mgosi, kumkamata na kumpeleka katika Kituo cha Polisi Wazo.

Baada ya kumuogesha binti yake, wakampeleka katika hospitali ya Mwananyamala alikochukuliwa vipimo kadhaa na kuambiwa wampeleke mtoto huyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Hospitalini walituambia kwamba sehemu zake za siri zimeharibiwa sana na hata kibofu chake cha mkojo pia kimeharibiwa kwani wametoa uchafu mwingi. Kwa sasa amelazwa hospitalini huku akiendelea kupatiwa matibabu na hawajajua ni siku gani ataruhusiwa.”

MTOTO AFUNGUKA
Waandishi wetu hawakuishia hapo, walimfuata mtoto na kumuuliza maswali kadhaa kwa lengo la kujiridhisha ambapo alisema:

“Mgosi alinichukua, akaniambia twende kwake, tulipofika huko akanivua nguo na kunilalia...ameniumiza,” alisema mtoto huyo huku akionekana bado kuwa kwenye maumivu makali.

Baada ya kumpeleka Mgosi katika kituo cha Wazo, aliwekwa rumande na kufunguliwa jalada la mashtaka WH/RB/1891/2014KUBAKA.

 NA Haruni Sanchawa, Nyemo Chilongani GPL
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm