Baadhi
ya misaada iliyoletwa na wageni waalikwa katika kusaidia familia Zaidi
ya 25 zilizokuwa katika mazingira magumu chini ya taasisi ya Nitetee.
Mama
Tizeba (kulia), Mke wa Naibu Waziri wa Uchukuzi ambae alikuwa mgeni
rasmi katika uzinduzi wa taasisi ya Nitetee wakifungua kwa pamoja pazia
na Bi Flora Lauwo (kushoto), Mkurugenzi na Muasisi wa Nitetee Foundation
kuashiria uzindizu rasmi wa taasisi hiyo katika hafla iliyofajiaka
Jumapili Jioni katika Ukumbi wa New Mwanza Hotel, jijini Mwanza.
Mtoto
Veronica ambae ni mmoja ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu
walioibuliwa na taasisi ya Nitetee akitoa ushuhuda wa maisha yake yeye
na wadogo zake baada ya baba yao kufungwa jela kwa kesi ya mauaji na
kasha mama yao kuwakimbia na kwenda kwa mwanaume mwengine. Kwa mujibu wa
Veronica anasema baba yao amefungwa kwa kusingiziwa kwani siku mauaji
hayo yakitokea baba yake alikuwa ndani anaumwa, na tukio hilo limezima
ndoto zote za maisha yake na wadogo zake.
Meya
wa Jiji la Mwanza Mh. Stanislaus Mabula (kushoto) akizungumza na wageni
waalikwa (hawapo pichani) na kumpongeza Mkurugenzi wa Nitetee
Foundation kwa moyo wake wa kujitoa katika kuwasaidia watu wenye
mahitaji maalum. Mh meya aliahidi kufanya kazi na taasisi hiyo katika
lengo la kutetea watu wengi Zaidi ambae nae alichangia magodoro sita.
Katikati ni Mshehereshaji wa hafla hiyo ambae ni Mtangazaji wa kituo cha
Start TV Bi. Ivona Kamonte na msanii H-Baba.
Kina mama wa jiji la Mwanza walihudhuria hafla ya uzinduzi wa jiji la Nitetee Foundation katika Hoteli ya New Mwanza.
Nguvu
imeongezeka katika jitihada za kusaidia jamii ya wanaoishi mazingira
magumu hapa nchini baada ya kuzinduliwa taasisi inayojishughulisha na
kutoa misaada ya kibinaadamu kwa wanawake na watoto walio kwenye
mahitaji makubwa hasa jamii ya vijijini na nje ya miji, inayojulikana
kama NITETEE FOUNDATION toka jijini Mwanza.
Shirika
hilo la maendeleo kwa ajili ya wanawake na watoto nchini Tanzania
lilizinduliwa usiku wa Jumapili na mgeni rasmi ambae alikuwa ni mke wa
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mama Charles Tizeba katika ukumbi wa New Mwanza
Hotel, iliyopo jijini Mwanza. Tukio hilo la aina yake lilipendezeshwa
na wenyeji wa mkoa wa Mwanza pamoja na watu maarufu kadhaa, viongozi wa
vyama na jiji la Mwanza akiwemo Stanislaus Mabula, Mwanamuziki Stara
Thomas na H-Baba, Katibu CCM mkoa wa Mwanza Bi Joyce Masunga.
Akiongea
na wageni walihudhuria katika uzinduzi huo Mgeni rasmi ambae ni Mke wa
Waziri wa Uchukuzi Mama Charles Tizeba aliwasihi wanawake nchini kutunza
familia zao na kutowaacha wakaitwa watoto wa mitaani.
“Wimbi
hili la watoto mpaka hii leo hata wengine kufikia hatua ya kuwaita
watoto wa mtaa kana kwamba wanazaliwa na mitaa tuna uwezo wa kuliondoa
endapo tu, wakina mama tutasimamia kwanza misingi ya walezi, ama wazee
wetu kwa kurudisha dhana ya ‘MTOTO WA MWENZIO NI WAKO PIA” alisema mama
Tizeba na kuhoji “haya maneno ya sugar mamy, sugar dady, sijui vidumu,
wamama haya maneno yanatoka wapi?”
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa NITETEE
Foundation Bi. Flora Lauwo amesema kwamba Taasisi ya NITETEE imekuwa
ikifanya shughuli zake za kuwasaidia watoto kutoka familia zenye kipato
cha chini vijijini na pembezoni mwa mji ili waweze kupata fursa ya
kupata elimu pamoja na wanawake kupata fursa za kujikwamua kiuchumi.
“Malengo
yetu ni kutoa na kuongeza kasi ya maendeleo hapa nchini hasa katika
sekta ya elimu. Hivyo basi miradi yetu italenga kuhamasisha jamii ya
kipato cha chini ambao hawawezi kuwapatia elimu watoto wao hasa maeneo
ya vijijini na pembezeno mwa miji na kupunduzo matatizo ya moja kwa moja
kwa jamii hizi pamoja na matatizo ya saikolojia wanazokumbana nazo
watoto, vijana pamoja na wanawake” alisema Mkurugenzi wa Nitetee Bi.
Flora
“Lengo
la Nitetee ni kufikia jamii zote za Tanzania nzima, kwa kuanza tumeanza
moja kwa moja kwenye ngazi ya familia ambapo tunamgusa mototo na mama
ama mlezi ambaye anasimamia kuleta ustawi wa mtoto huyu, tutahangaika
kwanza kubaini hizo familia zenye kusongwa na uduni wa maisha usio na
msaada, baada ya kujiridhisha tutaambatana na familia hizo kushirikisha
watanzania wengine kuona uhitaji huo ili kuweza kusaidia kwa namna Mungu
anavyotuwezesha watu wake.” aliongeza Bi. Flora.
Bi
Flora alimalizia kwa kusema kwamba “Kwa kuanzia taasisi hii mpaka sasa
tumetembelea familia 25 zote za kutoka hapa jijini mwanza, kati ya hizo
familia baada ya kuridhia, tumejitahidi kadri ya uwezo wetu kutoa
msaada ambao tulishirikiana na marafiki wachache tuliokuwa tukizungumza
nao juu ya hizo familia na kutoa mahitaji muhimu naya karibu kwa kadri
tulivyoweza kwa baadhi tu ya hizo familia” .
CHANZO:MO-BLOG
0 comments:
Post a Comment