Mahakama ya juu kabisa nchini India imefanya uamuzi wa kihistoria kwa kuruhusu kitengo cha jinsia ya tatu, ikisema kwamba watu wa jinsia mbili sasa wanaweza kujitambulisha hivyo kwenye vyeti rasmi nchini humo.
Wanaharakati wanasema uamuzi huo ni afueni kwa mamilioni ya watu wanaobaguliwa katika jamii yenye nadharia kali za kihafidhina nchini India.
Mahakama ya Juu ya ndia iliamuru serikali kuwamujuisha watu wa jinsia mbili katika mipango yote ya watu masikini, ikiwa ni pamoja na elimu, huduma za afya na nafasi za kazi ili kuwasaidia kupambana na changamoto za kijamii na kiuchumi.
Kabla ya uamuzi huo wa leo, watu wa jinsia mbili walilazimika kujitambulisha kama wanaume au wanawake katika nyaraka zote za serikali.
CHANZO:DW
0 comments:
Post a Comment