Wanaume wanaovua mashati wamepigwa marufuku kuitembelea bustani ya mapumziko na kujivinjari ya Adventure Island.
Ni eneo ambalo watu wanakwenda kujivinjari na familia zao, kwa kutazama wanyama, watoto hupata kubembea na pia watu huota jua.
Bustani hiyo iliyopo mjini Southend
nchini Uingereza, imeweka ilani zinazowaomba wanaume wasivue mashati
yao, na kwamba watakao patikana watafukuzwa.
Mkurugenzi mkuu, Marc Miller, amesema anataka wanaume waonyeshe "ustaarabu".
Bustani hiyo inasifika duniani kwa kuwa na idadi
kubwa ya watu walio uchi walioipanda bembea ya 'Rollercoaster' - licha
ya kwamba ni jambo linalofanyika faraghani.
'Kuilenga Familia'
Zaidi ya watu 100 walivua nguo ili kuipanda bembea hiyo ijulikanayo kama Green Scream mnamo 2010.
Miller anasema: "Katika miaka ya hivi karibuni,
tumekuwa tukiongeza idadi ya vijana na wanaume ambao huvua mashati yao
ili kupata joto la jua kwa wingi. Hilo ni sawa kabisa lakini katika
mazingira yanayofaa".
"Tunajaribu sana kufanya biashara inayoivutia familia na sio kila mtu anavutiwa kuona vifua wazi".
Pamoja na kuwa na idadi kubwa duniani ya watu
wasio vaa nguo, Adventure Island pia ilijaribu kuweka rekodi mpya ya
kuwa na watu wengi wanaocheza mpira wa gofu wakiwa uchi, mnamo mwaka
2012.
Msemaji mmoja anasema michezo yote hufanyika faraghani.
"Wanaohudhuria michezo hiyo ni waliojisajili
kushiriki, ili kuchanga fedha nyingi za misaada ya kukabiliana na
magonjwa kama saratani ya matiti na ya uume," alisema.
"Marufuku hiyo imetolewa wakati bustani imefunguliwa kwa umma."
CHANZO:BBC
0 comments:
Post a Comment