Mwanariadha wa Afrika kusini Oscar Pistorius amerejea tena
mahakamani kuhojiwa zaidi na kujibu maswali ya mwendesha mashtaka mkuu
Gerrie Nel katika kesi anayoshtumiwa kwa kumpiga risasi na kumuua mpenzi
wake mwanamitindo Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwezi februari tarehe
14 mwaka uliopita .
Bwana Nel amekuwa akimwandama Pistorius , akisema hakuwa mkweli katika toba yake na alimfokea mpenzi wake Reeva Steenkamp mara kwa mara .
Siku ya kwanza ya maswali ya mahakama dhidi yake Nel alianza kwa kuonyesha picha za kutisha za kichwa kilichochuruzika damu cha Bi Steenkamp, baada ya kupigwa risasi na Pistorius.
Mwanariadha huyo anadai hakumuua makusudi bali alidhani ni mtu alievamia nyumba yake.
Ameiambia mahakama kuwa alimpenda sana mwanadada huyo Reeva .
Kiongozi wa mashataka amemsuta Pistorious akisema kuwa alikuwa ni mbinafsi sana kwa mpenzi wake na kuwa kile alichokijali sana ilikuwa ni sifa zake na hadhi yake katika jamii.
Pistorious alikanusha madai hayo akisema anajuta kwanini hakuwahi kumwambia Reeva kuwa anampenda kupitia ujumbe wa simu ya mkononi.
SOMA ZAIDI

0 comments:
Post a Comment