Mkurugenzi
wa Uboreshaji Afya Wama, Dkt.Sarah Maongezi (Kulia) akiongea na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu ushirikiano
uliopo baina ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo pamoja na Jamuhuri ya
Watu wa China nchini katika kusaidia wananchi ikiwemo ziara
wanaoyotarajia kuifanya katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kuanzia tarehe 12
hadi 19 Aprili mwaka huu,Katika ni katibu wa Balozi wa China nchini,Ren
Zhihong na Meneja Mawasiliano wa Wama Philomema Marijani.
Katibu
wa Balozi wa Jamuhuri ya watu wa China nchini, Ren Zhihong (katika)
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano uliofanyika
maelezo jijini Dar es salaam kuelezea ushirikiano uliopo baina ya
Taasisi ya Wama na Ubalozi wa China katika shughuli za kusaidia
jamii.Kulia ni Mkurugenzi wa Uboreshaji Afya Wama ,Dkt.Sarah Maongezi na
kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Wama Philomema Marijani.(Picha na
Lorietha Laurence).
Na Lorietha Laurence
Taasisi
ya Wanawake na Maendeleo kwa kushirikiana na Balozi wa Jamuhuri ya
watu wa china nchini, Lu YouQing itafanya ziara kuitembelea mikoa ya
kanda ya ziwa kuanzia tarehe 12 hadi 19 Aprili mwaka huu kwa shughuli
za kusaidia jamii.
Akiongea
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa
Uboreshaji Afya ,Dkt.Sarah Maongezi amesema lengo la ziara hiyo ni
kusaidia jamii za watu wa kanda ya ziwa katika sekta za afya.elimu
pamoja na kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi.
“Lengo
kuu la ziara hii ni kuwasaidia wananchi wa mikoa ya Mara,Simiyu,kagera
na kigoma kwa kutoa huduma ya afya na elimu bure pamoja na kuwasaidia
wanawake waweze kujiinua kiuchumi ili kuimarisha ushirikiano wa
shughuli za maendeleo na uwekezaji”alisema Dkt.Maongezi.
Aliongeza
kuwa shughuli zitakazofanywa katika ziara hiyo ni kuwatambulisha
wataalamu wa afya kutoka china ambao watatoa huduma ya upimaji wa afya
na dawa bure katika hospitali ya wilaya ya Butima,na msaada ya
vyerehani kwa vikundi vya wanawake wajisiriamali pamoja na
vitabu,mabegi na mipira ya kuchezea.
“Wama
haiko kwa ajili ya wanawake na watoto wa kike tu bali inasaidia watu
wote wake kwa waume,kwasababu kila alipo mwanamke na mwanaume naye yupo
nyuma yake hivyo inawahusisha watu wote ingawa imejikita zaidi kwa
wanawake.”alisema Dkt. Maongezi.
Naye
katibu wa Balozi wa Jamuhuri ya watu wa china nchini Ren Zhihong
ameusifu uhusiano mzuri uliojengeka kati ya serikali ya Jamuhuri ya
watu wa china na Tanzania ilidumu kwa miaka 50, na kuahidi kuendeleza
ushirikiano huo katika k shughuri mbalimbali za kijamii.
Taasisi
ya Wama ipo chini ya uongozi wa Mhe. Mama Salma Kikwete na
imejidhatiti katika kuwawezesha wanawake na wasichana ili kujenga jamii
yenye afya,maendeleo na iliyoelimika, ikisimamia dira ya “Wanawake wa
Tanzania wanawezeshwa kuishi maisha bora”.
CHANZO:MO-BLOG
0 comments:
Post a Comment