Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kundi la Wabunge wa vyama
mbalimbali vya siasa walio marafiki wa Tanzania pamoja na wanachama wa
Britain and Tanzania Society (All Party Parliamentary Group on
Tanzania, and Britain Tanzania Society) katika mchapalo walioandaa kwa
heshima yake katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola
katika jengo la Durbur jijini London April 1, 2014.
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aipata picha ya kumbukumbu na baadhi ya
Wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa vya Uingereza walio marafiki wa
Tanzania pamoja na wanachama wa Britain and Tanzania Society (All Party
Parliamentary Group on Tanzania, and Britain Tanzania Society) katika
mchapalo walioandaa kwa heshima yake katika ofisi za Wizara ya Mambo ya
Nje na Jumuiya ya Madola katika jengo la Durbur jijini London April 1,
2014.
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akijaribu kuendesha mfano wa mtambo wa
kufundishia namna ya kuchimba mafuta katika visima vilivyo bahari kuu
(KCA Deutag Dart Drilling Simulator and Well Enginering System)
alipotembelea Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen, Scotland,
Jumanne April 1, 2014 akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya
kiserikali ya siku tatu nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa
Uingereza Bw. David Cameron.
Zaidi ya Watanzania 20 wamepata udhamini wa
kusoma katika chuo hicho kuanzia mwaka huu, ambapo watasomea fani
mbalimbali za sekta za mafuta na gesi.
Nyuma yake ni ujumbe
alioongozana nao ikiwa ni pamoja na Waziri wa Biashara, Viwanda na
Masoko wa Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui (kulia) na Waziri wa Nishati
na Madini Profesa Sospeter Mhongo (wa pili kulia) Wa pili kushoto ni
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe Peter Kallaghe, akifuatiwa na
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya katika Wizara za mambo ya nje na
ushirikiano wa kimataifa Balozi Dorah Msechu.
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospter Muhongo wakisindikizwa na Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Robert
Gordon mjini Aberdeen, Scotland, Jumanne April 1, 2014 alikotembelea
akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kiserikali nchini Uingereza
kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron. Zaidi ya
Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika chuo hicho mwaka huu,
ambapo watasomea fani mbalimbali za sekta za mafuta na gesi.
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ana ujumbe wake katika picha ya pamoja na
uongozi wa Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen, Scotland,
Jumanne April 1, 2014 akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya
kiserikali nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw.
David Cameron. Zaidi ya Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika
chuo hicho mwaka huu, ambapo watasomea fani mbalimbali za sekta za
mafuta na gesi. (PICHA NA IKULU).
0 comments:
Post a Comment