Ridhiwani
Kikwete akihutubia wakazi wa kijiji cha Tokamisasa wakati wa mkutano wa
kampeni za ubunge zinazoendelea ambapo aliwaambia kuwa atahakikisha
tatizo la wakulima na wafugaji kwa kuweka mpango bora wa matumizi ya
ardhi.
Ridhiwani
Kikwete akihutubia wakazi wa kijiji cha Tokamisasa wakati wa mkutano wa
kampeni za ubunge zinazoendelea ambapo aliwaambia kuwa atahakikisha
tatizo la huduma za afya linatatuliwa, kuboresha miundo mbinu elimu na
kurudisha michezo jimboni.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete akicheza muziki na
Miraji Mtaturu Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi wakati wa mkutano wa
kampeni za ubunge jimbo la Chalinze uliofanyika kwenye kitongoji cha
Mbuyu kijiji cha Tokamisasa kata ya Ubena Zomozi.
Sam wa Ukweli akitumbuiza kwenye kampeni za CCM zilizofanyika katika kijiji cha Tokamisasa kitongoji cha Mbuyu.
Mgombea
wa Ubunge wa jimbo la Chalinze CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akisalimiana
na wazee wa kijiji cha Tokamisasa wakati akiwasili kwenye kitongoji cha
Tuka Mjini tayari kwa kufanya mkutano wa kampeni.
Msanii wa Mashairi
Mwanahamisi Mohamed wenye ulemavu wa macho akiimba shairi linaloitwa
Changamoto wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge jimbo la Chalinze CCM
ambapo Ridhiwani Kikwete alihutubia na kuomba kura kwa wananchi wa
kijiji cha Tokamisasa.
Wakina
Mama wa Kimasai wakifuatilia kwa makini mkutano wa kampeni za ubunge za
CCM ambapo mgombea wa CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete alifika katika tawi
la Kivuga na kuomba kura.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wafugaji wa Kimasai
wa Tawi la Kivuga kata ya Ubena Zomozi wakati wa mkutano wa kampeni za
ubunge jimbo la Chalinze.
Mgombea
Ubunge wa CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akizungumza na vijana
wajasiriamali wa UVCCM mshikamano Visakazi mara baada ya kuzindua shina
hilo lililopo katika kata ya Ubena Zomozi.
0 comments:
Post a Comment