Home » » RAIS WA VICOBA TANZANIA AZINDUA VICOBA MKOA WA NJOMBE

RAIS WA VICOBA TANZANIA AZINDUA VICOBA MKOA WA NJOMBE

Written By kitulofm on Thursday, 10 April 2014 | Thursday, April 10, 2014

Kulia ni makamu wa Rais Vicoba Taifa Bi.Scolastika Kevela Akiwa na Rais wa VICOBA Tanzania Bi.Devotha Likokola
Rais wa Vicoba Tanzania na Mbunge wa Viti Maalum Jimbo la Peramiho Bi.Devotha Likokola Amewataka Wananchi Kutumia Vizuri Fursa Wanazozipata Katika Kujikwamua na Umasikini Katika Kujiunga Kwenye Vikundi Mbalimbali Vya Kijamii.

Akizungumza na Mamia ya Wanachama wa Vikoba Kutoka Katika Maeneo Mbalimbali ya Mkoa wa Njombe na Mkoa Jirani wa Ruvuma Bi.Likokola Amesema Kuwa Kila Mwana VICOBA Lazima Ahakikisha Anafanya Kazi ya Kuendeleza Vicoba Kwa Malengo Ili Kuweza Kufanikiwa Kupata Mkopo Mkubwa Utakaowawezesha Kuinua Uchumi Kiujumla.

Pamoja na Mambo Mengine Amewaagiza Wanachama Wote Pamoja na Viongozi Wake Kufuata Mfumo Rasmi wa Uendeshaji wa Vicoba Hivyo IIli Kuhakikisha Jamii Inanufaika na
vicoba Endelevu.

Katika Hatua Nyingine Amelaani Tabia Za Baadhi ya Watu Wanaojitokeza Mitaani Kuwadanganya Wananchi Kuanzisha Vikundi Visivyoendelevu Vinavyoweza Kusababisha Mifarakano Mikubwa Pindi Fedha Zitakapo Kuwa Zikipotea Bila Utaratibu.

Kwa Upande wake Makamu wa Rais VICOBA  Tanzania Bi.Scolastica Kevela Amewataka Akina Baba Kuwaruhusu Wake Zao Kujiunga na Vicoba Ili Waweze Kuacha Kumtegemea Baba Kwa Kila Kitu.

Awali Akisoma Taarifa Ya VICOBA Mkoa wa Njombe Mratibu wa Mafunzo ya VICOBA Mkoa wa Njombe Bi.Ester Mgeni Amesema Kuwa Licha  Ya Kuwa na Mtaji Unaofikia Zaidi Ya Shilingi Bilioni 1.8 Lakini Bado Kuna changamoto Mbalimbali Ikiwemo Upungufu wa Fedha Kwa ajili ya Mikopo Ya Kutosha Wanachama Wote.

Aidha Amesema Pia VICOBA Mkoa wa Njombe Bado Vinakabiliwa na Ukosefu wa Eneo la Kujenga Ofisi za VICOBA Pamoja na Kuwepo Kwa Dhana ya Baadhi ya Watu Kudhani VICOBA ni Vya Kisiasa.

Hata Hivyo Imetajwa Kuwa Hadi Sasa Kuna Zaidi Ya Wanachama Laki Tatu wa Vicoba,Vikundi Zaidi Ya Elfu Kumi na Hisa Zaidi Ya Shilingi Bilioni 3 Ambazo Zinawasaidia Wanachama Wake Katika Kuinu Uchumi Wao.

Na Gabriel Kilamlya, Njombe
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm