Wananchi wa kijiji cha Idende kata
ya Bulongwa wilayani Makete Mkoani Njombe wameamua kuivunja kamati ya ya maji
ya kijiji baada ya kukosa maji kwa zaidi ya mwaka mmoja hadi sasa
Katika hali ya vuta nikuvute
iliyochukua muda mrefu wananchi wameamua kuivunja kamati ya maji kijijini hapo
iliyokuwa na watu saba iliyokuwa ikiongozwa na mwenyekiti Bahati Sanga na
kuunda kamati mpya yenye watu nane kwa kuzingatia jinsia mbele ya Mkutano wa
Hadhara uliofanywa na wananchi zaidi ya 300
Maaumuzi hayo yamefanywa na wananchi
wa kijiji hicho baada ya kuwepo malumbano yasiyotajwa kiini chake kati ya Fundi
maji wa kijiji hicho na Kamati ya maji iliyonundwa kwa ajili ya kushughulikia
huduma ya maji kijijini hapo inapatikana kwa muda wote
Naye Afisa Mtendaji wa kijiji hicho
Bw.Elia Kyando amesema kuwa wananchi wameamua kuchukua uamuzi huo baada ya
kuona kumekuwepo malumbano kati ya Fundi maji na kamati hiyo na kusababisha
ukosefu wa maji ndani ya mwaka mzima hadi sasa
Bw.Jerald Tweve ambaye ni Fundi maji
katika kijiji hicho amesema kuwa tatizo la wananchi hao kukosa maji ni Uchakavu
wa Miundombinu ya maji iliyotokea katika kijiji cha jirani cha Imehe kata ya
Bulongwa hivyo maboresho ya haraka yanahitajika ili kuhakikisha wananchi
wanaipata huduma hiyo
Bw.Tweve Amewataka wananchi kuwa na
subira na kusema kwamba atafanya jitihada zake kuhakikisha wananchi hao
wanapata huduma ya maji ndani ya mwezi mmoja ujao
Na Furahisha Nundu
0 comments:
Post a Comment