Home » » WANANCHI WAASWA KUACHANA NA MATUMIZI YA VIPIMO VISIVYO RASMI

WANANCHI WAASWA KUACHANA NA MATUMIZI YA VIPIMO VISIVYO RASMI

Written By kitulofm on Wednesday, 9 April 2014 | Wednesday, April 09, 2014

DSCI0084
Mkuu wa Kitengo cha Sheria Toka Wakala wa Vipimo Bw. Moses Mbunda akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mchakato wa Kunazisha Sheria Mpya itakayosaidia kuimarisha Sekta ya Upimaji Nchini, Kulia ni Kaimu Meneja Sehemu ya Habari toka Wakala wa Vipimo Bi. Irene John.
DSCI0097
Meneje wa Upimaji toka Wakala wa Vipimo Bw. Richard Kadeghe akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ambavyo vipimo batili vinayotumika.
DSCI0103
DSCI0065
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano wa Wakala wa Vipimo leo Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO).
Na Frank Mvungi MAELEZO
Serikali yawatahadharisha wananchi kuhusu matumizi ya vipimo batili hususani visado na ndoo za Plastiki.
Hayo yamesema na Kaimu Meneja wa  Habari,Elimu na Mawasiliano  wa EWakala wa Vipimo Tanzania Bi Irene John wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akieleza Bi Irene amesema ufungashaji na upimaji batili ni kinyume cha sheria ya Vipimo sura 340 (iliyopitiwa mwaka 2002) pamoja na Kanuni zake.
Akifafanua zaidi  alisema ufungashaji na matumizi ya vipimo batili hudhoofisha uchumi wa Taifa kwa kuwa humpunja mkulima,mlaji,mfanyabiashara na mtumiaji.
Aliongeza kuwa Serikali imekuwa ikipoteza mapato yake ambapo Halmashauri hukusanya mapato pungufu wanapotoza ada kwa gunia badala ya uzito au ujazo.
Arene  alitaja athari nyingine kuwa ni kuathiriwa kwa biashara ya kimataifa kutokana na wananchi kutokuzingatia vipimo hasa kwa kutumia mizani wakati wanapofanya biashara ya kununua na kuuza.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya ufundi wa wakala huo bw.Peter Masinga alisema ni vyema wananchi wakaacha kutumia vipimo batili kwani vimekuwa vikidhoofisha ukuaji wa uchumi kwa muda mrefu na hivyo kwenda kinyume na jitihada za Serikali za kuwaletea maendeleo wananchi.
Bw. Peter aliongeza kuwa kuanzishwa kwa vituo vya kununulia mazao vijijini ni moja ya hatua zitakazosaidia kuondoa tatizo la vipimo batili kwa kuwa Serikali itaweza kusimamia kwa ukaribu matumizi ya vipimo sahihi kama vile mizani.
Wakala wa vipimo ni Wakala wa Serikali ambayo ilianzishwa Mei,2002 kwa Tangazo la Serikali namba 194 kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi, jukumu kuu likiwa kumlinda mtumiaji kupitia matumizi ya vipimo sahihi.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm