Home » » SHIRIKA LA TUNAJALI KUZINDUA MRADI WA ZERO VVU KWA MIKOA YA NJOMBE NA IRINGA

SHIRIKA LA TUNAJALI KUZINDUA MRADI WA ZERO VVU KWA MIKOA YA NJOMBE NA IRINGA

Written By kitulofm on Tuesday, 12 November 2013 | Tuesday, November 12, 2013


  Picha na Aminia website
Na Veronica Mtauka
 
Shirika la TUNAJALI linatarajia kuzindua mradi wa zero VVU katika mkoa Njombe na Iringa ili kutokomeza maambukizi mpya ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Hayo yamebainika mapema hii leo mjini Makambako mkoani Njombe kwenye kikao cha wadau na wanahabari wa vyombo vya habari vya mkoa wa Njombe na Iringa ambapo wanahabari hao wametakiwa kuwa chachu ya kutumia vyombo vyao vya habari katika kutoa elimu kuhusu tiba ya ART kwa maisha yote kwa wajawazito na wanaonyonyesha wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Katika kikao hicho imebainika kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kupunguza viwango vya maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Tanzania imelenga kutokomeza maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi miongoni mwa watoto na kuwafanya akina mama waishi kwa muda mrefu zaidi.

Mpango huu umezinduliwa na mh. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania DR.Jakaya Mrisho Kikwete mkoani Lindi siku ya Ukimwi duniani mwaka 2012 na umeadhimia kufikia malengo ya kutokomeza maambukizi hayo kutoka asilimia 26 mwaka 2011 hadi asilimia 4 ifikapo mwaka2015.

 
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm