Na Ergon Elly & Fadhil Lunati
MAKETE
Zoezi la Upimaji na Ugawaji wa Viwanja katika eneo la Soko Kuu Makete kwa wafanyabiashara
waliobomolewa Vibanda vyao kupisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami
wilayani Makete Mkoani Njombe limekamilika
rasmi hii Leo kwa Wafanyabiashara na Kukabidhiwa Viwanja hivyo kwa ajili ya
kuanza Rasmi Ujenzi Huo.
Hayo yamesemwa na Afisa Ardhi wilaya ya Makete Bw.
Anikas Vilumba wakati alipokuwa akifanya Shughuli ya Upimaji wa Viwanja Hivyo
kwa Wafanyabiashara na ameongeza kuwa Endapo wafanyabiashara watajitokeza
katika eneo hilo la Viwanja watakabidhiwa kwaajili ya kuanza Rasmi kwa Ujenzi
wa Vibanda vya Biashara kwa walio athirika na zoezi na bomoabomoa.
0 comments:
Post a Comment