Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), kimesema hakitakubali kura ya maoni za Katiba Mpya kufanyika
bila daftari la wapiga kura kuboreshwa.
Akihutubia mkutano wa hadhara Kijiji cha
Mwendakulima, wilayani Kaliua, mkoani Tabora, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk
Willibrod Slaa alisema hawatakuwa tayari kuingia kura ya maoni ya
Katiba Mpya bila daftari la wapiga kura kuboreshwa kwa kisingizio cha
gharama na ukubwa wa nchi.
Dk Slaa alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec)
haipaswi kuogopa gharama za kufanya mabadiliko hayo, huku akibainisha
kuwa demokrasia yenyewe ndiyo gharama na kwamba, kufanyia maboresho
daftari hilo ni matakwa ya sheria siyo hisani.
SOMA ZAIDI:MWANANCHI
SOMA ZAIDI:MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment