Zaidi ya wasichana 700 wenye umri kati ya miaka 10 na 19 ambao
walikatisha masomo kwa sababu ya mimba katika shule za msingi na
sekondari Wilaya ya Kahama, wamejitokeza kupatiwa elimu ya uzazi wa
mpango na ujasiriamali inayotolewa na Shirika la Kiota Women Health
Development (Kiwohede) la Dar es Salaam.
Idadi hiyo ni kubwa ikilinganishwa na wasichana
350 waliopo kwenye bajeti ya mradi, hali iliyoonyesha tatizo hilo kuwa
kubwa wilayani Kahama.
Mkurugenzi wa Kiwohede, Justa Mwaituka alisema
idadi hiyo ya wasichana 700 waliokatisha masomo imetoka kata nne za
Lunguya, Shilela, Mhongolo na Busoka kati ya kata 55 za Kahama, hali
ambayo inaonyesha ni hatari.
SOMA ZAIDI:MWANANCHI
SOMA ZAIDI:MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment