Hatimaye Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Olasiti, jijini
Arusha, lililopigwa bomu Mei 5, mwaka huu na kuahirishwa uzinduzi wake,
limezinduliwa jana na Balozi wa Papa na Mwakilishi wa Vatican nchini
Tanzania, Askofu Fransisco Padilla.
Kabla ya uzinduzi huo, ibada hiyo ilianza kwa kubariki makaburi
matatu ya Regina Laizer (50), James Kessy (16) na Patricia Assey (10),
ambao wote waliuawa katika tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment