Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Modesta
mkazi wa Ludewa amefariki dunia wakati akiwa njiani akikimbizwa katika
hospitali ya Mission Ikonda kulingana na tatizo la barabara ya Makete-Njombe
kuwa mbovu
Hata hivyo Mtu huyo aliyefariki dunia katika eneo
kulingana na tatizo la ubovu wa barabara na gari kushindwa kupita kirahisi
inasemekana kuwa hadi kufikia saa kumi na moja jioni kulikuwa na wagonjwa
waliokuwa katika hali mbaya
Taarifa hizo zimetufikia mara baada ya
barabara ya Makete Njombe eneo la Mang’oto kuanzia shule ya sekondari mang’oto
hadi getini kutopitika hali inayopelekea wasafiri kushindwa kushindwa kufika
kwa wakati katika eneo husika
Kwa taarifa za awali inaonyesha kuwa kuna
wakandarasi wanakuja kufanya ukarabati ambapo nao wamekwama eneo hilo ikiwa tatizo kubwa ni kifusi kilichosambazwa katika
eneo hilo ambapo hadi kufikia jioni ya leo gari
zaidi ya 10 zilikuwa zimekwama katika eneo hilo
0 comments:
Post a Comment