Home » » KINANA KUWASILI LEO WILAYANI MAKETE

KINANA KUWASILI LEO WILAYANI MAKETE

Written By kitulofm on Thursday, 5 December 2013 | Thursday, December 05, 2013


Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Bwana Hosea Mpagike Akizungumzia Ratiba ya Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdurlahman Kinana na Msafara Wake Mkoani Njombe.
 
Na  Gabriel  Kilamlya Njombe
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Abdurlahman Kinana Anatarijia Kuwasili Mkoani Njombe leo Jioni Kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Mbili Ikiwa ni Muendelezo wa Ziara Yake ya Kutembelea Kukagua Miradi Mbalimbali ya Maendeleo.

Ujio wa Katibu Mkuu wa Chama Hicho Bwana Kinana Umelenga Kukagua Shughuli Mbalimbali Zinazofanywa na Vijana Katika Maeneo Mbalimbali Pamoja na Chama cha Mapinduzi CCM Ikiwa ni Pamoja na Kuhakikisha Serikali Inatekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010/2015 Kama Inavyosema.

Akizungumzia Juu ya Ziara ya Kiongozi Huyo wa Kitaifa,Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Bwana Hosea Mpagike Amesema Kuwa Bwana Kinana Pia Ataongozana na Viongozi Mbalimbali wa Chama Akiwemo Mbunge Mteule Dokta Asha Rose Migiro Pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Ndugu Nape Mnauye.


Bwana Mpagike Amesema Kuwa Kinana Ataanzia Ziara Yake Wilayani Makete Katika Mkoa wa Njombe Ambapo Disemba 6 Mwaka Huu Atakuwa Wilayani Hapa Katika Vijiji Mbalimbali na Kukagua Shughuli Mbalimbali za Vijana Kisha Kuwasili Mjini Njombe Majira ya Jioni Siku Hiyo.

Akiwa Mjini Njombe Katibu Mkuu Kinana Atazindua Mradi wa Kitega Uchumi wa CCM na Kufanya Mkutano wa Hadhara Katika Uwanja wa Roman Catholic Karibu na Benki ya CRDB Hapo Disemba 7 Mwaka Huu.

Katika Kipindi Hiki Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Kupitia Katibu Wake Mkuu Kimeendelea Kufanya Zaiara Katika Mikoa Mbalimbali Ambapo Hadi Sasa Msafara Huo Utawasili Mkoani Njombe Ukitokea Jijini Mbeya.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm