Home » » WAKAZI WA NJOMBE WAMEMFUKUZA MWENYEKITI WA KIJIJI

WAKAZI WA NJOMBE WAMEMFUKUZA MWENYEKITI WA KIJIJI

Written By kitulofm on Thursday, 5 December 2013 | Thursday, December 05, 2013

HUYU NI MWENYEKITI WA KIJIJI BWANA HOSEA MPOSOLA ALIYEFUKUZWA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA ITULAHUMBA WAKISEMA HAWANA IMANI NAE


  Na  Michael Ngilangwa
   
Hatimae sakata la wananchi wa kijiji cha Itulahumba la kuwakataa viongozi limeingia sura mpya baada ya wananchi hao kumufukuza mwenyekiti wao na kumuchagua mwenyekiti wa muda huku wakimuomba mkurugenzi kumuondoa afisa mtendaji ambae amepelekwa hivi karibuni kusimamia maendeleo ya kijiji hicho.


Wakiongea mbele ya viongozi wa kata na taarafa ya Mdandu wananchi hao wameelezea sababu za kumkataa mwenyekiti wa  kijiji hicho bwana Hosea Mposola kwa kuruhusu afisa mtendaji aliyekuwepo bwana Method Mligo kuhamia kijiji cha Itambo  bila kusoma hesabu za mapato na matumizi,kuruhusu afisa mtendaji mpya kuhamia katika kijiji hicho pasipo wananchi kufahamishwa uwepo wake jambo lililopelekea wananchi kutokuwa na imani na mwenyekiti huyo.

Kuhusu afisa mtendaji aliyehamishiwa katika kijiji hicho akitokea kijiji cha Itambo bwana Batista Msemwa wananchi hao wamesema kuwa hawamuhitaji mtendaji huyo kutokana na wananchi wa kijiji cha Itambo kumkataa kutokana na kutuhumiwa kuhusika na   ubadhilifu wa mali za kijiji cha Itambo na kwamba serikali  imekuwa na tabia ya kuwahamishia vijiji vingine watumishi wanaotuhumiwa na ubadhilifu wa mali za wananchi ili waendelee na ufujaji wa mali za wananchi.

Akizungumza kwenye mkutano  wa hadhara afisa taarafa ya Mdandu bwana Benson Wanderage amesema kufuatia kuteuliwa kwa mwenyekiti wa muda wananchi wanatakiwa kuonesha ushirikiano katika kutekeleza miradi ya kijiji hicho huku akisema kuwa serikali ya kata itakwenda kumuagiza afisa mtendaji aliyehamishwa arudi kijijini hapo ili asome  taarifa ya hesabu za mapato za matumizi.

Diwani wa kata ya Mdandu bi Anna Upendo Gombela amesema  amewapongeza wananchi kwa  mahudhurio ya wananchi hao na kwamba  lengo la kuwakutanisha wananchi hao ni kutatua mgogoro uliokuwepo baina ya viongozi na wananchi  wa kutokuwa na imani na uongozi wa kijiji  akiwemo mwenyekiti huku akisema wajumbe wa  serikali ya kijiji wameridhia kufanya uteuzi wa mwenyekiti wa muda ambae anakubalika na wananchi wote.

Afisa mtendaji wa kata ya Mdandu bwana Timoth Fute amesema kuwa ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe tayari imechukua  hatua za kumuandikia barua yakwenda kusoma hesabu za mapato na matumizi ya kijiji cha Itulahumba   mtendaji huyo pindi atakapo pona kwani kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Kibena ambapo ameahidi kumsimamia ili kuhakikisha anakwenda kusoma taarifa za mapato na matumizi ya kijiji hicho ndipo  aweze kuhama.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm