Home » » MBUNGE PINDI CHANA AKABIDHI FEDHA ZAIDI YA MILLIONI MOJA NA VIFAA KWA VIONGOZI WA UWT WILAYANI MAKETE

MBUNGE PINDI CHANA AKABIDHI FEDHA ZAIDI YA MILLIONI MOJA NA VIFAA KWA VIONGOZI WA UWT WILAYANI MAKETE

Written By kitulofm on Sunday, 29 December 2013 | Sunday, December 29, 2013



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh2m8vZLvGZou4LRghH-UI-8xtZnelbPm0YolHU_J8-uQ6n00hDj5A5uudcyT_L8oDhOplc_mu3oezqnWWeSxT8ZwKBhdqahC9P7VSNjVXdsfsde31R5o1o7LCko6of5EgeqJuO36k8rRP_/s640/IMG_7648.jpgMbunge wa viti maalum Mkoa wa Njombe na mjumbe wa NEC Taifa Bi.Pindi Chana ametoa kiasi cha sh.milioni moja laki 4,majembe,vitenge pamoja na karenda kwa viongozi wa UWT Wilaya ya Makete kwa lengo la kuwaendeleza akina mama wa Makete kiuchumi.

Akizungumza na baraza UWT Wilaya ya Makete Bi.Pindi Chana amesema akina mama wananafasi kubwa  ya  kuleta  maendeleo katika jamii na hivyo kama  Taifa litaelekeza nguvu kwa akina  mama umasikini unaweza kufika kikomo.

Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya  Makete Bi.Safi Almasi amevitaja vitu vilivyotolewa kuwa ni pamoja na fedha zilizo tolewa  na Bi.Chana na kuongeza kuwa kiongozi huyo amekuwa ni mfano wa  kuigwa hapa nchini na wilayani Makete

Katika baraza hilo pia kulihudhuliwa  na mjumbe wa Chama Cha Mapinduzi (w)Bw.Ona Sukunala Nkwama ambaye pia amemshukuru Mh.Pindi Chana kwa kuwajali wanawake nchini ikiwa  ni pamoja na  kuwatembelea katika wilaya ya Makete

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm