Mkandarasi kutoka kampuni ya Boimanda Nickson Makyao akizungumza namna atakavyotekeleza makubaliano yake na kijiji
Mwenyekiti wa kijiji cha Mago, Paulo Sanga akitoa maelezo yake
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro(kushoto) akiangalia jinsi sehemu ya barabara hiyo ilivyoharibika
Tingatinga lililozuiwa na wananchi lisiondoke
Hali
ya sintofahamu iliyokuwa imetanda katika kijiji cha Mago wilayani
Makete kufuatia wananchi wa kijiji hicho kuzuia kuondolewa kwa mtambo
uliokuwa ukitumika kuchimba na kupakia kifusi, imemalizika kufuatia
mazungumzo yaliyofanyika kijijini hapo
Mazungumzo hayo yamewahusisha Mkuu wa
wilaya ya Makete mh. Josephine Matiro, mkandarasi, TANROADS mkoa wa
Njombe pamoja na viongozi wa kijiji hicho cha Mago
Akizungumza
kwenye kikao hicho mwenyekiti wa kijiji cha Mago Bw. Paulo Sanga
amesema wakati mkandarasi huyo akichimba kifusi, walikubaliana kuwa
mkandarasi huyo atatengeneza maeneo ya barabara yatakayoharibika wakati
malori yakipita na kifusi pamoja na kusomba lori mbili za matofali mpaka
sehemu iliyoandaliwa
Bw.
Sanga amesema kilichosababisha wakauzuia mtambo huo maarufu kama
tingatinga ni baada ya kuona kuwa wanakuja kuuchukua bila kutekeleza
makubaliano waliyoyafanya awali, na kuongeza kuwa wanaimani angechukua
vifaa vyake asingerudi kutengeneza
Mkandarasi
wa kampuni ya Boimanda inayolalamikiwa aliyejitambulisha kwa jina la
Nickson Makyao amesema si kweli kwamba amekataa kutekeleza makubaliano
hayo, na badala yake amesema walitakiwa kuhamisha mtambo huo ili
ukaendelee kufanya kazi sehemu nyingine, huku ukarabati huo ukiendelea
Bw.
Makyao amesema atabeba matofali hayo kama walivyokubaliana pamoja na
kukarabati maeneo yote ya barabara hiyo yaliyoharibiwa wakati
wakipitisha kifusi, na kuongeza kuwa kwa sasa bado wataendelea kutoa
kifusi katika kijiji hicha na kukipitisha kwenye barabara hiyo lakini
kabla hawajafanya hivyo, watairekebisha na kuendelea kupitisha kifusi na
endapo itaharibika tena wataikarabati sehemu walizoharibu
majibu
hayo yalionesha kuleta furaha kwa wajumbe wa kikao hicho, na kuonekana
na nyuso za furaha kwani ndicho walichokuwa wakitaraji kukisikiliza
Pia
mkandarasi huyo ametoa rai kwa wananchi kuacha tabia ya kuzuia mitambo
kwani kwa kufanya hivyo kunakwamisha shughuli za kimaendeleo hasa ya
ujenzi wa barabara katika maeneo mengine hali itakayoleta usumbufu kwa
wananchi wote
Naye
mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro amewatoa hofu wananchi hao
kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa mapema iwezekanavyo na kuwa na imani
na mkandarasi huyo kwani amekuwa akifanya kazi zake kwa uaminifu
Jana
Desemba 10 wananchi hao walizuia kuchukuliwa kwa tingatinga lililokuwa
likitumika kuchimba na kupakia kifusi kuondolewa kijijini hapo kwa madai
kuwa makandarasi hakutekeleza makubaliano baina yake na kijiji.
Na Edwin Moshi
0 comments:
Post a Comment