Kamanda
wa polisi mkoa wa njombe kamishna Msaidizi mwandamizi wa polisi bwana furgence
Ngonyani ametoa wito kwa vyombo vya habari kushirikiana na dawati la jinsi la
polisi kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kulitumia na kupunguza vitendo
unyanyasaji wa kijinsia.
Wito
huo ameutoa mapema hapo jana kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Makete alipokuwa
anazungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya ukaguzi na tathimini
katika tarafa na kituo cha polisi Makete.
Aidha
kamanda Ngonyani amesema kuwa jeshi la polisi limejipanga kupambana na vitendo vya
unyang`anyi wa kutumia silaha uporaji wa pikipiki ambao wa Mkoa wa Njombe
matukio ya kupora na mauji kwa madereva wa pikipiki ni machache ukilinganisha
na sehemu nyingine
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Makete ambae
pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya Makete Bi.Josephin
Rabi Matiro amemshukuru Kamanda Ngonyani kwa kuimarisha ulinzi kwa kupeleka
polisi kwenye tarafa na kuwaomba wananchi wawatumie huko tarafani.
0 comments:
Post a Comment