Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amewasili nchini Afrika Kusini usiku wa kuamkia
leo Desemba 10, 2013 tayari kuhudhuria maziko ya Rais Mstaafu wa Afrika
Kusini Mzee Nelson R. Mandela.
Kwa
mujibu wa taarifa rasmi ya serilai, Ibada Kuu ya kumwombea Marehemu
itafanyika leo Desemba 10, 2013 katika Uwanja wa FNB Johannesburg,
ambapo viongozi na watu mashuhuri mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia
wataungana na wananchi wa Afrika Kusini katika shughuli hiyo ya
kihistoria.
Kesho
Novemba 11 hadi Novemba 13, 2013 mwili wa marehemu utakuwepo katika
jengo la Union Building ambapo viongozi na watu mashuhuri watatoa
heshima zao za mwisho. Jengo hilo ni kama Ikulu ya nchi hiyo.
Maziko yatafanyika Desemba 15, 2013 katika kijiji cha Qunu, Mthatha, Easter Cape.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Waterkloof
Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria alikowasili usiku wa
kuamkia leo tayari kuhudhuria mazishi ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini
Mzee Nelson R. Mandela.
Rais
Kikwete akisalimiana na Mwambata wa Kijeshi katika Ubalozi wa Tanzania
Afrika kusini katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko
Kusini mwa jiji la Pretoria
Rais
Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa
ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria .
Nyuma yake mwenye ushungi kichwani ni Mama Salma Kikwete
Rais
Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa
ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria .
Nyuma yake kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahman Kinana.
PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment