Home » » VOLCANO KUBWA DUNIANI YAGUNDULIWA CHINI YA BAHARI

VOLCANO KUBWA DUNIANI YAGUNDULIWA CHINI YA BAHARI

Written By kitulofm on Wednesday, 11 December 2013 | Wednesday, December 11, 2013

Volcano yenye ukubwa wa Ubelgiji (Belgium) imegunduliwa kwa mara ya kwanza, na jopo la wanasayansi chini ya bahari ya Pacific. wanasayansi hao, wamegundua kuwa mwamba huo mkubwa ulitokana na mlipuko wa lava, na kuifanya volcano hiyo mpya kuwa sio tu ni kubwa duniani, bali ni kubwa katika solar system-kubwa kuliko Olympus Mons (iliyoko mars.)


Tamu Massif Iko juu ya plateau kubwa iliyoko Km 2 chini ya maji, kaskazini-kusini mwa bahari ya pacific ya mashariki ya Japan,volcano hiyo yenye ukubwa wa sq Km 310,000 (119,000 sq m) haina madhara wanasayansi hao wamesema. Mara ya mwisho kuripuka ilikuwa ni chini ya maji, miaka milioni 142 iliyopita wakati wa kipindi cha mwisho cha Jurassic, kabla binaadam kuumbwa
Utafiti uliochapishwa katika "Nature Geoscience unaonyesha kuwa formation zaidi ya miamba mikubwa chini ya maji inaonekana kuwa ni matokeo ya volcano kubwa zilizokufa zamani
 
credit: djfetty
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm