Home » » RAIS WA TANZANIA JAKAYA KIKWETE AZUNGUMZA KATIKA MAZISHI YA MANDELA HII LEO

RAIS WA TANZANIA JAKAYA KIKWETE AZUNGUMZA KATIKA MAZISHI YA MANDELA HII LEO

Written By kitulofm on Sunday, 15 December 2013 | Sunday, December 15, 2013


mandela

Mazishi ya mzee Nelson Mandela katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Eastern Cape na kumaliza wiki moja ya maombolezi ya shujaa huyu wa Afrika 


 Idadi ya Takribani watu 4,500 wakiwemo wageni wa kimataifa wamehudhuria mazishi hayo yanayoendelea sasa hivi ambayo ni ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa.

Familia ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi ya leo huku kukiwa na muimbaji ambaye atakuwa anaita mizimu ya mababu wa kale huku wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa anazikwa.
1483139_563742170368160_40127197_n
Moja kati ya mataifa yaliyopata heshima ya kuongea mbele ya viongozi mbalimbali duniani ni Rais wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Eneo analozikwa mzee Nelson Mandela ni sehemu ya  makaburi yaliyo kwenye shamba kubwa la familia ya Mandela lililoko katika kijiji cha Qunu lililojengwa mara baada ya kuachiliwa kutoka jela mwaka 1990, katika eneo lenye nyasi za kijani , na milima ya Cape ya mashariki.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm