Watoto
wawili wenye umri wa miaka tisa,wamechomwa moto viganja vyao vya mikono
na baba zao katika wilaya ya Newala mkoani Mtwara.
Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku kumi na sita
za kupinga ukatili wa kijinsia hapa nchini, ITV kwa kushirikiana na
chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA waliamua
kufuatilia tukio la ukatili waliofanyiwa watoto hao kwa kuchomwa moto
viganja vya mikono yao na baba zao walowazaa kwa kumtafuta kwanza afisa
ustawi wa jamii wa wilaya ya Newala bwana George Martin Shinganya ili
kueleza walichofanyiwa watoto hao katika vijiji tofauti vya wilaya hiyo.
ITV ililazimika kumtafuta mwalimu mkuu wa shule ya
msingi Mwongozo katika kijiji cha Makonga kata ya Nambunga bwana Nurdin
Machemba,na kueleza kuwa alishughulikia suala la mtoto huyo kama
mwanafunzi wake na kisha kukabidhi uongozi wa serikali ya kijiji
kuendelea nayo lakini mtuhumiwa amekimbilia nchi ya Msumbiji hivyo
kuomba serikali kusaidia ili akamatwe.
chanzo:ITV
0 comments:
Post a Comment