Taswira ya picha eneo la tukio
Inaeleza
kuwa Ndege ya abiria aina ya Boeing 787 ya shirika la ndege la Ethiopia
(Ethiopian Airlines) mchana siku ya jana imeshindwa kutua kwenye Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka na hitilafu iliyokuwepo Uwanjani
hapo na kulazimika kutua kwa dharura kwenye Uwanja wa Mdogo wa Arusha,hali
iliyopelekea Ndege hiyo kusimama nje kabisa ya uwanja huo huku abiria zaidi ya
200 wakiwa ndani ya ndege hiyo bila ya kushuka.
Wataalam
wa Ndege wapo eneo la tukio kutafakari
namna watakavyoweza kuwashusha abiria hao na kutafuta namna ya kuweka sawa
mambo ili Ndege hiyo iweze kuruka.
Tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu tukio hilo,na
tutaendelea kufahamishana kadri taarifa itakavyokuwa ikitufikia.
0 comments:
Post a Comment