Hii ndiyo hali halisi ya ajali iliyokuwa pikikipiki imekuwa katika hali mbaya
Katika
hali ambayo ni ya majonzi ajali ya pikipiki usiku wa kuamkia leo saa
4:22 usiku Kta ya Iwawa Makete mjini eneo maarufu kama Kona watu wawili
wamegongana uso kwa uso na pikipiki(BODABODA)
Katika
ajali hiyo pikipiki yenye namba T 280 BJR na nyingine ni T 878 BUK ,na
majeruhi walili waliojeruhiwa vibaya katika maeneo ya kichwa ambapo
majeruhi hao ni madereva wa pikipiki hizo walitambuliwa kwa jina moja
moja la Ndondola na Mwangadele walifikishwa katika Hospitali ya Wilaya
Makete kwa msaada wa wasamalia wema ili kuokoa maisha yao
Kwa
mujibu wa mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio wamesema kuwa
ajali hiyo imetokea katika eneo baya lenye kona japo kuwa kama madereva
hao wangekuwa makini ajali hiyo isinge tokea
Hata
hivyo hadi kitulo fm imefika eneo la tukio polisi walifika mapema na
kuweza kuchukua pikipiki hizo kwa kusaidiana na mashuhuda waliokuwepo na
kuzipeleka katika kituo cha polisi wilaya ya Makete
Kwa
taarifa iliyotufikia hivi punde isiyo rasmi na chanzo chetu ya habari
ni kwamba mtu mmoja ameumia vibaya katika kichwa chake hivyo amepelekwa
katika hospitali ya Rufaa Mkoani Mbeya kwa matibabu zaidi
Kwa habari zaidi endelea kutembelea mtandao huu
Na Furahisha Nundu
0 comments:
Post a Comment