Hali ya usala
ma katika wilaya
ya Makete kwa msimu wa sikukuu za Krismas kwa mwaka 2013 na Mwaka mpya 2014
imeenda vizuri bila matatizo
Akitoa taarifa hiyo kwa
wanahabari mapema hii leo ofisini kwake Mkuu wa polisi Wilaya ya Makete
(OCD)Alfred Kasonde amesema kuwa msimu wa Krismas na mwaka mpya umeenda vizuri
kwani hakuna tukio lolote la uvunjifu wa Amani lililoripotiwa katika kituo
hicho
Hata hivyo katika mazungmzo
hayo amesema kuwa wananchi na wakazi wa wilaya ya Makete wamesherehekea sikukuu
hizo kwa amani,upendo na mshikamano kama
ilivyotegemewa
Pia amesema kuwa Jeshi la
polisi wilayani Makete lilijipanga vyema kuhakikisha amani inapatikana muda
wote kwani Doria kutoka kwa jeshi hilo
ilikuwa ikifanyika kwa msimu wote wa sikukuu hizo
Hivyo Kasonde
amesemewashukuru wananchi kwa kusherehekea sikukuku hizo kwa kufuata taratibu
na sheria bilashuruti kwani ni wajibu wa kila mmoja kulinda amani pamoja na
kuwa na ushirikiano katika jamii inayotuzunguka
Hata ametoa wito kwa wananchi
wilayani hapa kuendeleza amani,mshikamano pamoja na upendo na kuongeza kuwa
Jeshi limejipanga kuhakikisha kuwa amani
inapatikana kwa wakati wote kuanzia mwaka 2014 na kuendelea
Na Furahisha Nundu
0 comments:
Post a Comment