Akikabidhi
msaada huo Meneja mahusiano kwa wateja wa Benki ya NMB-Makete Bw.Ally Sheyo
amesema kama wafanyakazi wa benki hiyo
wameamua kutoa msaada kwa watoto hao kwa sababu kituo hicho kinategemea misaada
kutoka kwa wahisani
Mahitaji
yaliyotolewa ni pamoja na mafuta ya kupikia,unga,sabuni na sukari ,Hata hivyo
ametoa wito kwa taasisi binafsi na zile za serikali kutembelea kituo hicho kwani kinakabiliwa na
changamoto mbalimbali.
Kwa
upande wake Mlezi wa watoto hao Bi.Sekela Nkyami ametoa shukrani kwa Benki
hiyo kwa moyo waliouonyesha na kuongeza
kuwa anashukuru kwa msaada huo kwani kituo hicho kinaendeshwa kwa msaada wa
Sister Anna ambaye anajitahidi kuomba misaada kwa wahisani na hakuna fungu
lolote kutoka serikalini.
Pia
ameongeza kuwa watu wa ustawi wa jamii wawe karibu na kituo hicho kwani ni
wajibu wao kukitembelea kituo na kujitahidi kuomba misaada serikalini,kwa
wahisani pamoja na kuwafikishia walengwa mara misaada hiyo ifikapo ili
kuwasaidia watoto hao.
Na Fadhili Lunati
0 comments:
Post a Comment