Home » » KIJIJI CHA TANDALA AMBACHO NDIO MAKAO MAKUU YA KATA HAKINA OFISI YA KIJIJI

KIJIJI CHA TANDALA AMBACHO NDIO MAKAO MAKUU YA KATA HAKINA OFISI YA KIJIJI

Written By kitulofm on Monday, 6 January 2014 | Monday, January 06, 2014



Kijiji cha Tandala kinatarajia kuanza ujenzi wa ofisi ya Mtendaji wa kijiji kutokana na ukosefu wa jingo la ofisi
ya kijiji kwa muda wa miaka mingi ambapo hivi sasa linatumika jengo la posta Tandala kama ofisi ya kijiji.

Ujenzi huo unaanza mapema mwaka huu eneo la mtaa wa Singida  ambapo mpaka kufikia sasa uwanja umepatikana tayari  kwa ujenzi kuanza.

Akizungumza na mwandishi wa habari  Afisa mtendaji wa kijiji hicho ambaye pia ni kaimu Afisa mtendaji kata ya Tandala Bw.Ambele Sanga amesema kuwa ofisi hiyo itaanza kujengwa mapema mwaka huu

Amesema kuwa kila kitongoji kinatakiwa kuchangia nguvu kazi ikiwemo kufyatua tofali 1500 ili ziweze kutumika katika ujenzi huo na kusema kuwa kijiji hicho kinavitongoji 6

Pia amevipongeza vitongoji ambavyo tayari vimekwisha kuaandaa tayari tofali ikiwemo kitongoji cha Utsewa na Lwangilo 

Katika hatua nyingine Bw.Sanga amesema kuwa wanampango wa kujenga Intenki katika mradi wa maji Utsewa pamoja na kuboresha miundombinu ya kitongoji cha Utsewa na kilovoko ikiwa ni pamoja na kutoa miti ya kigeni na kupanda miti ya asili katika vyanzo vya maji

Na Henrick Idawa

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm