Huyu ndie Msanii aliyekutwa amejinyonga katika nyumba ya kulala wageni Tanga
Baadhi ya wasanii waliokuwa na msanii huyo picha chini aliyekaa katika kochi ni marehemu enzi za uhai wake
umati wa wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo

Mtu mmoja ambae ni msanii amekutwa amejinyonga katika nyumba ya kulala wageni (gesti house) ijulikanayo kwajina safari juonir iliyopo kisosora jijini tanga.
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa tanga Costantino Masawe amesema mtuhuyo amefaamika kwa jina la victar Peter ambaye amejinyonga kwa kutumia mkanda wake wa Suruali ndani ya chumba chake ambacho alikuwa kodisha yeye na wenzake waliyo kuwa wakiandaa filam yao.
Kamanda masawe amesema chanzo cha tukio hilo akijafahamika kwasasa wanaendelea kutafuta chanzo chake, na amesema marehemu alikuja jijini tanga na wasanii wenzake kwaajili ya kuandaa filam kwani ila kwa uchunguzi mdogo waliyofanya kikundi hicho cha akijasajiriwa na bali walikusanyana na wasanii wadogo na wakubwa filamu yao. Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali kuu ya bombo iliyopo jijini hapa.
Hata hiyo kamanda huyo akusita kuwahasa wakazi wa jiji la tanga kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi mkoani hapa ilikuweza kukabiliana na matukio ya uvunjifu wa amani bali kila mtu azingatie kutii sheria bila shuruti kwa kufanya hivyo itasaidia kukomesha vitendo vya kialifu.
saluti kwa dullonet
0 comments:
Post a Comment