Kutokana na wilaya ya Makete kuwa miongoni
mwa wilaya chache hapa nchini kuzalisha kwa wingi matunda aina ya matofaa
maarufu kama apples, halmashauri ya wilaya ya
Makete imeamua kushirikiana na wadau kupanua wigo wa kilimo hicho ili kizidi
kuleta tija kwa wakulima
Hayo yamebainika kufuatia kampuni ya TAHA
yenye makao yake jijini Arusha ambayo inahusika na uboreshaji wa mazao ya
bustani kufika wilayani Makete na kujadiliana kwa pamoja na halmashauri hiyo na
kuweka mikakati ambayo itasaidia kushirikiana kwa pamoja kuboresha kwa kiasi
kikubwa kilimo cha matofaa(apples)
Akizungumza hivi karibuni, Bwana Shamba wa TAHA Bw.
Manfred Mitala amesema wiaya ya Makete imekuwa ikifanya jitihada nyingi za
kuinua kilimo hicho hivyo ujio wao utasaidia kuboresha na kuongeza nguvu za
pamoja katika kuboresha kilimo hicho
Bw. Mitala amesema mwaka jana rais Kikwete
alipofanya ziara wilayani Makete alifurahishwa na taarifa iliyotolewa na
halmashauri kuwa kilimo cha apple kinapatikana pia wilayani hapo, hivy aliagiza
kilimo hicho kiboreshwe zaidi kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali, na
ndiyo maana halmashauri hiyo imeanza kutekeleza agizo hilo kwa kushirikiana na shirika lake
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya ya Makete mh. Daniel Okoka amesema kwa kuanzia shirika hilo litafanya kazi kwenye kata 12 za wilaya
ya Makete ikiwemo kata ya Iniho na kuongeza kuwa kata nyingine ambazo watafanya
nazo kazi zitatangazwa hivi karibuni pindi utekelezaji utakapo anza
0 comments:
Post a Comment