Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) zimewaagiza wanachama wake- vyama vya mpira wa miguu vya
mikoa kuwapatia orodha ya klabu zote za mpira wa miguu zilizosajiliwa katika
mikoa yao .
Orodha hiyo inatakiwa
kujumuisha namba ya usajili wa klabu, viongozi waliopo madarakani kwa sasa
pamoja na mawasiliano yao
(namba za simu na anuani za email) na eneo yalipo makao ya klabu husika.
Kwa utaratibu huo,
vyama vya mikoa vitakusanya taarifa za klabu zinazocheza ligi ya mikoa, lakini
wakati huo vinatakiwa kuwasiliana na wanachama wake (vyama vya wilaya) kupata
taarifa za klabu zinazocheza ligi za wilaya na baadaye kuziwasilisha TFF.
Klabu ambazo taarifa
zake zitakuwa hazijawasilishwa TFF hadi Agosti mwaka huu hazitaruhusiwa
kushiriki ligi ya msimu wa 2014/2015 katika ngazi yoyote ile.
0 comments:
Post a Comment