Wito umetolewa kwa wananchi
wa wilaya ya makete katika kuchangia ujenzi wa maabara katika shule za sekondari zinazo wazunguka wananchi ili
kuongeza kiwango cha elimu wilayani makete na Tanzania kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Afisa mtendaji
wa kata ya mang’oto bw,Clemensi sanga,akiwa ofisini kwake huku akieleza kuwa
kwa mwaka 2014 kata hiyo
imejipanga kuhakikisha kata hiyo inachangia loli 30 za mawe katika ujenzi wa
maabara katika shule ya secondary Mang’oto lengo likiwa ni kuinua kiwango cha
taaluma katika masomo ya sayansi,na kupata wataalamu wa sayansi wilayani hapa
na nchini.
Bw,Sanga amesema kuwa sambamba
na mipango hiyo shule hiyo inakabiliwa na changamoto mabalimbali ikiwemo nyumba
za kuishi walimu,vyoo na bwalo kwa ajili ya kutumia wakati wa kula chakula.
Kwa upande wa wananchi wa
kata ya mang’oto wame ishukuru halmashauri ya (w) ya makete kwa juhudi walizo
fanya katika kuhakikisha miundombinu ya
shule hiyo pamoja na walimu wanapatikana tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.
0 comments:
Post a Comment