Mkurugenzi mtendaji wa
harmashauri ya (w) yamakete bw,Iddy nganya ametoa rai kwa wannchi wa makete
kuto jichukulia sheria mkononi pindi kunapokea sintofahamu juu ya uwajibikaji
wa watendaji katika shughuri za kimaendeleo.
Akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Malembuli katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika kijiji cha malembuli kilichopo katika kata ya mang’oto
katika kutafuta suluu ya mzozo ulio ibuka baina ya wananchi na afisa mtendaji wa kijiji Bw, Nganya,amesema
watendaji wote wanawajibu wa kusoma mapato na matumizi kwa wananchi ili kujua
hali ya maendeleo katika eneo husika.
Sambamba na hatua hiyo Mkurugenzi wa Harmashauri ya (w) ameeleza umuhimu wa kusoma mapato na matumizi na
kuwataka wananchi kutowafumbia macho viongozi wanao fanya kazi kwa uzembe kwa kuwa
wao ndio wasimamizi wa shughuli za maendeleo
Katika mkutano huo ulio udhuriwa na viongozi wa kijiji kata
na wananchi kwa ujumla ajenda ya mkutano
huo ilikuwa ni kutafuta suluu ya mzozo ulio ibuka mwanzoni mwa mwezi wa kwanza
mwaka huu ambapo wananchi wali taka kusomewa mapato na atumizi ya kijiji na trekta kwa kipindi cha zaidi ya miezi 6 hawaku somewa mapato na matumizi.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji
ambaye ndiye aliye tuhumiwa kutosoma mapato na matumizi amekiri kutokea kwa
ucheleweshaji na kwamba sababu zilizopelekea kutosoma mapato na matumizi kwa kipindi
hicho ni matatizo ya kifamailia ikiwemo misiba 3 iliyo mpata kwa kipindi hicho.
Aidha watu sita wakiwemo vijana
wameyakimbia makazi yao
kwa kuhofia kukamatwa na jeshi la polisi
kwa tuuma za kuvuruga mkutano wa kijiji siku hiyo ya tukio.
0 comments:
Post a Comment