Moja
ya kati ya Nyumba tatu zilizoathirika na upepo mkali uliovuma na
kuathiri nyumba mbali mbali katika Mtaa wa Kwaalamsha Mjini Zanzibar.
Jamii
Nchini imetahadharishwa kuwa makini katika kipindi hichi kilichoanza
cha msimu wa mvua za masika ambacho kimezoeleka kuwa na matukio mbali
mbali ya maafa yanayoleta athari kwa wananachi.
Tahadhari
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi wakati akiwafariji wananchi waliokumbwa na maafa
kufuatia Upepo Mkali ulioambatana na mvua jana jioni katika maeneo ya
Kwaalamsha, Makadara na Mkele ndani ya Wilaya ya Mjini.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapa pole baadhi ya
Wananchi ambao nyumba zao zilikumbwa na upepo mkali katika Shehia za
Kwaalamsha, Makadara na Mkele Wilaya ya Mjini.
Balozi
Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema mbali ya
mvua na upepo lakini kipindi hichi cha masika pia hukumbwa na miripuko
ya maradhi tofauti ya kuambukiza jambo ambalo jamii inapaswa kujihadhari
nayo.
Aliwahakikishia
wananchi hao kwamba Serikali Kuu kupitia Idara yake ya Maafa ambayo iko
chini ya Ofisi yake inaendelea kufanya tathmini na hasara iliyowakumbwa
wananchi hao na baadaye iangalie namna ya kusaidia nguvu
zitakazowawezesha kurejea katika mazingira yao ya awali.
Balozi
Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar
akiangalia jengo la Duka la Mfanyabiashara Khadija Ame Abdulla katika
Mtaa wa Kwaalamsha ambalo limeangukiwa na nguzo ya umeme kufuatia Upepo
mKali uliovuma katika eneo hilo.
“
Nimekuja na Timu yangu Katibu Mkuu, Mkurugenzi Maafa na timu yake kuanza
tathmini na maafa haya na baadaye kuandika ripoti itakayotusaidia sisi
Serikalini namna ya kuchukuwa hatua za kukabiliana na maafa hayo
yaliyojitokeza “. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi mbali mbali
waliojitolea nguvu, maarifa na hata hifadhi ya dharura kwa wenzao
waliopatwa na maafa hayo kufuatia upepo huo wa ghafla.
Alisema
kitendo hicho mbali ya kuleta faraja kwa waathirika hao pamoja na
Serikali kwa jumla lakini pia kimeongeza upendo na kuimarisha
ushirikiano na mshikamano miongoni mwa Wananchi hao.
“
Ukweli nimefarajika sana kusikia kwamba majirani zenu walikuwa pamoja na
nyinyi muda wote wa tukio hili. Huu hasa ndio ujirani mwema unaotakiwa
kuwemo ndani ya nyoyo za wanaadamu wakati wote “. Alifafanua Balozi
Seif.
Baadhi
ya nyumba zilizoathirika kutokana na upepo Mkali uliovuma na
kusababisha hasara kubwa katika Shehia ya Makadara Mjini Zanzibar.(Picha
na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ).
Wakitoa
shukrani zao kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi baadhi ya wananchi hao walioathirika na upepo huo walielezea
kufarajika kwao na hatua zilizochukuliwa na majirani zao katika
kuwasaidia kukabiliana na maafa hayo.
Nyumba
zipatazo Tatu katika Shehia ya Kwaalamsha, Tano Sheria ya Mkele na
nyengine kadhaa ambazo bado idadi yake hajijajuilikana katika Shehia ya
Makadara zimeathirika kutokana na upepo huo.
CHANZO:-MO BLOG
0 comments:
Post a Comment