Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete
(kushoto) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mindukene,Kata ya
Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 18,2014.Katika Mikutano
yake kwenye Vijiji vya Mindukene, Msigi na Kisanga ndani ya Jimbo
hilo,Ridhiwani Kikwete ameahidi kuhakikisha vijiji vyote kwenye jimbo
hilo vinakuwa na matrekta ili kuboresha kilimo.(Picha na Othman
Michuzi).
MGOMBEA
wa Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Jimbo la Chalinze
wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete ameahidi kuhakikisha
vijiji vyote kwenye jimbo hilo vinakuwa na matrekta ili kuboresha kilimo
kiwe na tija.
Alitoa
ahadi hiyo wakati wa mikutano ya kampeni kwenye vijiji vya Mindukene,
Msigi, Kisanga vyote vikiwa kwenye kata ya Talawanda.
Kikwete
alisema kuwa wakulima wengi bado wanatumia jembe la mkono ambalo
haliwezi kuwaletea manufaa wala kuboresha kilimo ambacho ni tegemeo lao.
“Nikianikiwa
kupata ubunge nitahakikisha kila kijiji kinakuwa na matrekta kwa ajili
ya kuwa na wakulima ambao wataweza kulima kwa faida kwa ajili ya chakula
na ziada kuuza ili kujiongezea kipato,” alisema Kikwete.
Akizungumzia
changamoto ya migogoro ya wakulima na wafugaji alisema kuwa
atahakikisha anazikutanisha pande zote ili kujua chanzo cha migogoro
hiyo.
“Tatizo
kubwa ni viongozi kushindwa kuzikutanisha pande zinazohusika badala
yake wanaongea na upande mmoja jambo ambalo haliwezi kumaliza migogoro
hiyo ambapo njia pekee ni kuwa na matumizi bora ya ardhi kwa kutenga
maeneo kwa wakulima na wafugaji,” alisema Kikwete.
Aidha
alisema kuwa migogoro hiyo inatokana na wafugaji kuingia kinyemela
pasipo kufuata taratibu bila ya kupitia kwenye mikutano mikuu ya
serikali za vijiji.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete
akifurahia jambo na Mzee Joseph January wa Kijiji cha Kisanda,Kata ya
Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze.(Picha na Othman Michuzi).
Katika
hatua nyingine aliwataka wazazi kuepukana na tabia ya kuuza kiholela
maeneo yao hali ambayo itasababisha vijana kukosa ardhi kwa ajili ya
kilimo na makazi.
Aliongeza
kuwa atahakikisha anaboresha masuala mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu,
afya, miundombinu, kilimo, mikopo kwa vijana na akinamama, uzinduzi
rasmi wa kampeni unatarajiwa kufanyika kesho Aprili huko Chalinze na
uchaguzi utafanyika Aprili 6 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment