Home » » MABOMU YASIKIKA KWENYE MACHIMBO NZEGA, MBUNGE DKT KIGWANGALA AKAMATWA NA POLISI

MABOMU YASIKIKA KWENYE MACHIMBO NZEGA, MBUNGE DKT KIGWANGALA AKAMATWA NA POLISI

Written By kitulofm on Monday, 24 March 2014 | Monday, March 24, 2014

Wachimbaji wakiandamana leo wilayani Nzega mkoani Tabora.
 
Jeshi  la polisi wilayani Nzega mkoani Tabora limetumia nguvu kusambaratisha maandamano ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu yaliyolenga  kupinga kufungwa kwa machimbo yao ya Mwashina yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania Limited wilayani Nzega.
Mara baada ya kukaribia katika eneo la machimbo ambako maandamano yalikuwa yanaelekea,kabla hata hawajafika eneo la machimbo,ghafla polisi waliibuka na kuanza kurusha mabomu hovyo na baadaye kumkata mbunge wa jimbo la Nzega Dkt Hamis Kigwangalla ambaye kabla ya kuanza kwa maandamano hayo alifanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nzega ndogo ili kujua mstakabali wa wachimbaji hao ambao hivi karibuni waliziuiwa kuchumba na kamishana wa madini nchini Paul Masanja kwa kile kilichotajwa kuwa wamevamia eneo hilo.

Kufuatia malalamiko ya wachimbaji hao kuondolewa bila kujali gharama waliozotumia walimwomba mbunge wao aridhie maandamano hadi katika eneo la machimbo ndipo mkutano ukavunjika na maandamano yakaanza na matokeo yake mabomu ya machozi pamoja na risasi za moto.
Katika  na purukushani hizo polisi walifanikiwa kumkamata mbunge huyo na kumjeruhi mtu mmoja kwa risasi ya moto kwenye paji la uso ambapo waliondoka nae kwenye gari pamoja na mbunge huyo.


Katika hatua nyingine hali ilikuwa tete kwa waandishi wa habari kwani askari wa jeshi hilo waliziba njia na kuwazuia waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa vitisho mbalimbali na matumisi ingawa hali hiyo ilitulia baada ya maandamano ya wachimbaji kujitokeza.

CHANZO:EDDY BLOG
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm