Jana majira ya sita mchana hadi saa kumi na moja jioni katika barabara iendayo uwanja wa ndege wa kimataifa KIA Kilimanjaro International Airport kumetokea machafuko pata shika vuta nikuvute shati kuchanika rubega kufumuka..!
Takribani
kama masaa mawili usalama ulipotea baada ya Wamasai kudai kufukuzwa
katika makazi yao wakiambiwa ni eneo la uwanja wandege.
Wamasai hao waliamua kuzuia magari yalioelekea Uwanjani hapo huku wakisema kuwa
hata wamiliki wa uwanja huo nao wahame kwani waliwakuta awali wakiishi hapo.
Polisi na magari ya PT
walifika katika tukio hilo na kutaka kumaliza migogoro hiyo kisheria
ila wamasai wamesema endapo muafaka utalenga kuwakandamiza hawako tayari
kuhama.
CHANZO:EDDY BLOG Imeripotiwa na DJ TINDO WA UTS TAIFA KILIMANJARO
0 comments:
Post a Comment