Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa
wa Njombe RTO James Kiteleki Akizungumza na Baadhi ya Viongozi wa
Daladala na Taxi Mjini Njombe Ofisini Kwake.
Mwenyekiti wa Daladala Mkoa wa Njombe Bwana
Seleman Mwenda Akitolea Ufafanuzi wa Kero Wanazo zipata Toka Kwa
Madereva wa Taxi za Kusalaliza na Bajaji Mjini Njombe
Jeshi
la Polisi Mkoani Njombe Kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani Kwa
Kushiririkiana Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji Wa nchi Kavu Na
Majini SUMATRA Imepiga Marufuku Utumiaji wa Namba Za Magari ya
Binafsi Katika Shughuli za Kibiashara na Kuwataka Kupeleka Orodha Ya
Majina ya Madereva wa Taxi "Wanaosalaliza" Ili Kuweza Kuwachukulia Hatua
Madereva Hao.
Akiongea
Kwenye Kikao na Wakuu wa Vituo Vya Daladala, Bodaboda na Taxi Kamanda
wa Kitengo Cha Usalama Barabarani RTO James Kiteleki Amesema Kuwa
Kutokana na Kufanyika kwa Vikao Vingi Vyenye Kujadili Suala Hilo
Hivyo ni Muda Wa Kila Mtumiaji Wa Vyombo Vya Moto Kufuata Sheria.
Katika
Hatua Nyingine Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoa Wa Njombe Bi Mary
Menard Amewataka Wale Ambao Hawajakidhi Masharti Ya Kuendesha Vyombo
Vya Moto Kupaki Vyombo Hivyo Ikiwemo Kuwa na Namba ya Chombo Yenye
Rangi ya Njano.
Kwa
Upande Wao Baaadhi ya Viongozi wa Vituo vya Daladala na Taxi na
Bodaboda Licha ya Kuliomba Jeshi Hilo Kusogeza Muda Mbele Ili
Kuwawezesha Wamiliki wa Vyombo Hivyo Kujipanga Lakini Baadhi Yao Akiwemo
Kiongozi Wa Daladala Wameonyesha Kulalamikia Madeleva Taxi Ambao
Wamekuwa Wakisalaliza Wateja na Kusababisha Abiria Kutokaa Kwenye
Vituo Maalumu vya Kupakia Abiria.
Kwa
Upande Wake RTO Akilijibia Suala Hilo Amewataka Viongozi wa Vituo Vya
Taxi Kuwasilisha Majina ya Madeleva Wote Ambao Wamekuwa Wakivunja
Utaratibu Uliowekwa wa Kupaki katika Vituo Ili Kuweza Kuwashughulikia.
Chanzo:Eddy blog
0 comments:
Post a Comment