Na Mwandishi wetu,
JUZI
tarehe 18/03/2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini
Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha kwenye Bunge maalum la Katiba
rasimu ya pili ya katiba.
Taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi imesema toka
awasilishe rasimu ile bungeni, kumekuwa na maombi mengi sana ya kutaka
kujua kama msimamo wa CCM juu ya baadhi ya mambo hasa muundo wa muungano
bado ni uleule.
Taarifa
hiyo imesema kwasababu ya maombi hayo CCM imeona bora kueleza kwa mara
nyingine tena msimamo na imani ya CCM juu ya swala zima la Muungano na
muundo wake.
Kimsingi
CCM ndio waasisi wa Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar. CCM
inamasilahi makubwa na mapana na Muungano huu kama waasisi pengine
kuliko taasisi nyingi ndani na nje ya nchi yetu.
Bado
CCM inaamini changamoto za Muungano huu suluhisho lake sio kubadili
muundo wa Muungano bali ni kuufanyia maboresho muundo wa muungano
tulionao wa serikali mbili. Hivyo basi CCM bado inaamini muundo bora
kwasasa utakao dumisha muungano wetu ni muundo wa SERIKALI MBILI.
Kwakuwa
kazi ya Warioba na Tume yake sasa imekwisha rasmi, kuisha kwa kazi yao
ni mwanzo wa awamu nyingine ya mchakato huu. Mwisho wa kazi ya Tume sio
mwisho wa mjadala juu ya Katiba tuitakayo bali ni mwanzo wa awamu
nyingine ya mjadala mpana na maboresho kama sio marekebisho ya kuondoa
mapungufu kwenye rasimu iliyowasilishwa.
Mwanzo
wa awamu hii nyingine ni furusa nzuri ya kupima kama kweli yaliyomo
kwenye rasimu na maelezo ya ziada yaliyotolewa na Jaji Warioba yana
akisi maoni ya Watanzania walio wengi.
Taarifa
hiyo ilisisitiza kwamba CCM ina amini awamu mbili zilizobaki kwakuwa
zinahusisha wawakilishi wa wananchi kupitia Bunge maalum la Katiba, na
hatimaye itawahusisha wananchi wenyewe moja kwa moja kupitia kura yao,
zitatumika vizuri kutupa ni nini hasa matakwa ya Watanzania juu ya
Katiba waitakayo na sio maoni au matakwa ya wachache.
Wakati
haya yote yakiendelea CCM bado tunaamini Muungano huu ni muhimu
ukadumishwa na kuimarishwa. CCM tunaaamini ili Muungano huu udumu njia
pekee kwasasa ni kufanya marekebisho kwenye Muundo wa serikali mbili ili
ujibu vizuri zaidi changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na kukidhi
mazingira ya sasa.
Taarifa
ilimalizia kwamba CCM inawaomba wanaCCM na watanzania kwa ujumla kuwa
watulivu katika kipindi hiki. Ni vizuri Watanzania
tukavumiliana,tukashindana kwa hoja tukitanguliza mbele uzalendo na
masilahi ya kweli ya nchi yetu.
CHA
0 comments:
Post a Comment